Habari rafiki yangu?
Umeianzaje siku yako ya leo?
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu.
Ikiwa ni siku nyingine nzuri kwetu ni Fursa ya pekee kwetu kwenda kuweka Akili,Nguvu na Maarifa ili tuweze kupata matokeo yaliyo bora zaidi.
Asubuhi ya leo tutafakari juu ya KAWAIDA..
Fikiri kawaida,chukua hatua kawaida,Weka juhudi Kawaida alafu Ukategemea matokeo tofauti hii inakuwa na maana gani?
Umefanya kama ambavyo kila mtu anafanya,Huna utofauti,Hujitumi na Unategemea kuwa na matokeo ya tofauti hii inakuwa na maana gani?
Kawaida ndio mwonekano na maisha ya wengi wanao ishi maisha kwa bahati nasibu au hata Kuwa na mpangilio wa hovyo wa matumizi ya muda wao yaani wanafanya vitu kama Dhalula au hajui kwamba itakapo tokea basi nitafanyaga hapo hapo,
hivi nani anashindwa kuishi mtindo huu rahisi kabisa?
Ukweli ni kwamba watu hawapendi kabisa kujitesa,
Watu hawapendi kabisa kujiweka tofauti,
Watu hawapendi kabisa kubadilika ila wanapenda kupata matokeo tofauti.
Rafiki ikiwa utachukua hatua ambazo kila mtu anachukua kwa nafasi yake yaani hatua rahisi na unategemea kupata matokeo tofauti huo utakuwa ni ujinga wa hali ya juu,
Kwa sababu tunavuna tulicho panda huwezi kupata mtama alafu ukavuna mahindi,Huwezi kupanda uvivu halafu ukavuna mafanikio makubwa huku ni kujidanganya.
95% ya watu wote Duniani wanapenda kufanya kawaida na kuishi kawaida yaani hawapendi kujitesa kwa lolote ndio maana watu wenye maisha ya kawaida ya kula kulala,Kujenga viota nk ni wengi kuliko maelezo,
Huku 5% pekee ndio watu wanao fanya mambo tofauti,Wanachukua hatua kubwa na kuweka juhudi kubwa na kupata matokeo makubwa ndio huishi maisha ya tofauti sana yaani Matajiri.
Hivyo rafiki iwapo utafanya kawaida kama kila mtu anavyo fanya usitegemee wala kuweka tumaini kwenye hilo na kwamba labda itatokea bahati na sibu ya kufikia mafanikio makubwa,
Mafanikio yoyote yanakutaka wewe uwajibike kikamilifu hivyo anza kuondoka kwenye kundi la 95% la kufanya kawaida na Anza kujijengea tabia za watu wa kundi la 5% kufanya tofauti kuweka juhudi kubwa Nk.
Fahamu kuwa ili kufanikiwa kuna marafiki lazima itakubidi kuwaachilia, kuna vitu unavyovipenda sana itabidi kuviachilia, maraningine itakulazimu kuhama na kwenda kuanza upya sehemu nyingine.
Utashangaa wengine wanafanikiwa na wewe unawaangalia tu, yamkini tatizo nipale ulipo, labda wao wapo sehemu sahihi na wewe haupo sehemu sahihi. Nikushauri kitu cha muhimu, usihame au kubadili mazingira kwa kuiga, hakikisha unaisikia sauti ya ndani ikikushawishi kufanya hivyo, take the leading of the Holy spirit ili kufanya maamuzi sahihi otherwise utakuja kujuta.
Wako katika kuijenga imani yako juu ya kufanikiwa maishani,
SENIOR MENTOR & PASTOR,
-Paul Biswalo.
Mhamasishaji,Muelimishaji,Mkufunzi na Mwalimu wa maswala ya maisha,uchumi,afya,utawala bora na mafanikio katika maisha.
Nifuate kwenye ukurasa wangu /ubao wangu ninaoandikia na kufundishia masomo mbalimbali juu ya maisha na mafanikio kupitia:https://www.linkedin.com/…/paul-biswalo-655a95…/.......kisha jiandikishe ili uwe wa kwanza kupata habari njema ya mafanikio.
Barikiwa sana wewe ujifunzaye kupitia hii habari njema ya juu ya kutimiza ndoto zako.
SENIOR MENTOR & PASTOR,
-Paul Biswalo.
Mhamasishaji,Muelimishaji,Mkufunzi na Mwalimu wa maswala ya maisha,uchumi,afya,utawala bora na mafanikio katika maisha.
Nifuate kwenye ukurasa wangu /ubao wangu ninaoandikia na kufundishia masomo mbalimbali juu ya maisha na mafanikio kupitia:https://www.linkedin.com/…/paul-biswalo-655a95…/.......kisha jiandikishe ili uwe wa kwanza kupata habari njema ya mafanikio.
Barikiwa sana wewe ujifunzaye kupitia hii habari njema ya juu ya kutimiza ndoto zako.
Hakuna muujiza hapo bila shaka utavuna na kukifurahia ulicho panda.
Kila la kheri rafiki yangu na mafanikio Mema.
No comments:
Post a Comment