Kuna watu wengi sana ambao kamwe hawatoweza kufikia ndoto zao kwasababu ya kuona kila kitu ni kigumu. Labda na wewe ni mmoja wao. Watu wahivi kila akiambiwa au kushauriwa kitu lazima ataanza kuwaza au kusema "ni ngumu" au "sidhani kama nitaweza", "fulani na fulani walijaribu wakashindwa".
Kwanini useme ni ngumu kabla haujajaribu?? Hivi unadhani kwenye maisha kuna vitu vinajijia tu pasipo jitihada? Nyie ndio mnataka kulishwa na kutunzwa na kukaa tuuu mnasahau kwamba there is no free lunch!!! Kwangu mimi maana ya ngumu ni "ongeza jitihada kidogo, ongeza nguvu kidogo hadi ufanikiwe".
Utakuta mtu anasema kila kitu kigumu wakati ni mwanamke na anawatoto, nikuulize, kwani ulipoenda kujifungua ilikuwa rahisi?? Mbona ulipoambiwa sukuma uliweza kusukuma na mtoto ukarudi naye nyumbani? Leo unaambiwa jaribu biashara hii unasema ngumu, fanya hivi au vile unalia eti "ngumu", basi kufa, uone kama nahiyo ni rahisi. Jifunze na ubadilike.
Shida kubwa ya wengi wetu kutokufanikiwa katika yale tuyafanyayo ni tabia ya kukosa kumaanisha, hatuna commitment katika mambo yetu ingawa kila mmoja ana kiu ya kufanya kitu. Kuwa na kiu, kuwa na lengo, kuhamasika ni kitu kimoja lakini commitment ni kitu kingine kabisa.
Hamasa yako na malengo yako na mbinu zako zote hazitakupeleka sehemu kama hautomaanisha kwenye kile unachokifanya. Commitment ndio ile nguvu ikiyoko ndani inayokusukuma kusema "ni ngumu lakini nitafanya",
"nimeshindwa mara kadhaa lakini nitajaribu tena", "lazima nione matokeo kwenye hili jambo kwa namna yoyote ile". Commitment ndio ile hali inayokufanya utembee kwenye lengo lako hata kama wengi wanakukatisha tamaa na kukurudisha nyuma. Mtu mwenye kumaanisha hakatishwi tamaa wala hazuiwi na kitu, sio mtu wa kutoa visingizio wala kulaumu hovyo, hata kuwepo na vizingiti na wengi wakate tamaa yeye atatafuta mpenyo tu.
Bishop Idahosa wa Nigeria aliwahi kusema "What a committee can not do, commitment can do". Natamani uanze leo kuwa committed katika uyafanyayo then uone mabadiliko yatakavyokujia.
BAADHI YA VITU VITAKAVYOKUSAIDIA KUJIPANGA MWAKA 2018
A. Kibinafsi
1. Jitathmini tabia zako na madhaifu yako
2. Angalia matumizi yako ya muda
3. Tathmini aina ya marafiki ulionao
4. Je watu wanakuitaje, wanamuchukuliaje, wanakusemaje?
5. Acha tabia za kulaumu, kulalamika na kuwa negative kwenye kila kitu
B. Kimaendeleo
1. Weka malengo
2. Weka mtandao bora, juana na watu wenye manufaa sio watu hasara
3. Jifunze kuweka akiba ya fedha hata kama nikidogo
4. Weka vipaumbele kwenye mambo yako. Be focused
5. Maanisha kwenye unayofanya. Be commited
6. Nunua unavyovihitaji sio unavyovitaka. Acha tamaa kwenye matumizi
C. Kimapenzi na kifamilia
1. Maanisha kwenye mapenzi. Usimchukulie poa mwenzako
2. Kuwa thabiti kwenye jukumu lako la kupenda au la kuheshimu. Maanisha
3. Kuwa na muda wa faragha na mume/mkeo
4. Pata muda na watoto wako
5. Boresheni mawasiliano baina yenu
6. Shirikishaneni mambo, hata yahusuyo pesa
7. Wote muwe na lengo la kuboresha penzi lenu sio kutegeana
Remember, whatever problem you're facing right now, is TEMPORARY. Nothing lasts forever, even pain and tears will eventually pass. If you learn to be flexible with your solutions and approach to difficult times, you'll always win!
- Paul Biswalo.
Wako katika kuijenga imani yako juu ya kufanikiwa maishani,
SENIOR MENTOR & PASTOR,
-Paul Biswalo.
Mhamasishaji,Muelimishaji,Mkufunzi na Mwalimu wa maswala ya maisha,uchumi,afya,utawala bora na mafanikio katika maisha.
kwa maelezo na kujifunza zaidi ,pitia hapa: https://paulbiswalomotivationalspeakingtalks.blogspot.com/
Meet you at the top. Heri ya mwaka mpya rafiki Rafiki zangu.
No comments:
Post a Comment