Ukiona kila jambo unalolifanya unasifiwa tu upo sahihi, na makofi mengi sana tuu bila kukosolewa jua unachokifanya bado hujakifanya kama inavyotakiwa. Nikufungue kitu kimoja muhimu hapa, ukitaka kujua unachokifanya kinakupeleka katika njia yako sahihi utaona makofi yanapungua lakini chuki, masimango , kukosolewa , kuonekana kama umechanganyikiwa kutaongezeka sana tuu.
Unachotakiwa kukifanya katika nyakati hizi ni ujipigie makofi kwa hatua kama hii alafu ongeza kasi kwa yale ambayo wanakusimanga nayo au hawakuelewi nayo vizuri. Mwaka 2018 uwe ni mwaka wa kuheshimu wenzako ili nao waheshimu uhalisia wako. Uwe ni mwaka wa kusimama katika imani ya yale unayoyafanya na sio kutikiswa na watu kusema wanakujua zaidi ya wewe unavyojijua.
Ni kanuni halisi kabisa kwamba katika maisha mara nyingine tunashindwa kufanikiwa au kuendelea au kupiga hatua kimaisha kwasababu tu ya maeneo tuliyomo na mazingira tunayoishi (Geographical locations). Wako watu kwenye vitabu vitakatifu ili wao kufanikiwa Mungu aliwaambia wahame walipo au wabadili mazingira ya watu wanaowazunguka na baada ya hapo maisha yao yakabadilika kabisa.
Fahamu kuwa ili kufanikiwa kuna marafiki lazima itakubidi kuwaachilia, kuna vitu unavyovipenda sana itabidi kuviachilia, maraningine itakulazimu kuhama na kwenda kuanza upya sehemu nyingine. Utashangaa wengine wanafanikiwa na wewe unawaangalia tu, yamkini tatizo nipale ulipo, labda wao wapo sehemu sahihi na wewe haupo sehemu sahihi. Nikushauri kitu cha muhimu, usihame au kubadili mazingira kwa kuiga, hakikisha unaisikia sauti ya ndani ikikushawishi kufanya hivyo, take the leading of the Holy spirit ili kufanya maamuzi sahihi otherwise utakuja kujuta.
Wako katika kuijenga imani yako juu ya kufanikiwa maishani,
SENIOR MENTOR & PASTOR,
-Paul Biswalo.
Mhamasishaji,Muelimishaji,Mkufunzi na Mwalimu wa maswala ya maisha,uchumi,afya,utawala bora na mafanikio katika maisha.
nifuate kwenye ukurasa wangu /ubao wangu ninaoandikia na kufundishia masomo mbalimbali juu ya maisha na mafanikio kupitia:https://paulbiswalomotivationalspeakingtalks.blogspot.com/.......kisha jiandikishe ili uwe wa kwanza kupata habari njema ya mafanikio.
Barikiwa sana wewe ujifunzaye kupitia hii habari njema ya juu ya kutimiza ndoto zako.
No comments:
Post a Comment